Shule ya Sekondari St. Monica Wasa inayomilikiwa na Masista Wamisionari wa Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu- Iringa, ilianzishwa rasmi tarehe 21/03/2019. Shule ni ya bweni na inapokea wa wanafunzi wa jinsi zote yaani wakike na wakiume, bila kujali dini, kabila, rangi au tofauti yoyote ile.
St. Monica sekondari inatoa elimu ya sekondari (Ordinary Secondary Education - O'Level) yaani kuanzia kidato cha kwanza (Form I) mpaka kidato cha nne (Form IV).
Shule ina mazingira mazuri na tulivu ya kujifunzia ikiwemo madarasa ya kutosha, maabara zenye vifaa toshelevu, maktaba ya kisasa yenye vitabu vya kutosha na Walimu mahiri watakao mlea mwanao kitaaluma na kimaadili...
Soma zaidi
Shule ya St. Monica Wasa Sekondari imejitofautisha katika nyanja mbalimbali kwa kutoa elimu bora kwa watoto wote, kujikita katika ujenzi wa kizazi chenye kuleta manufaa kwa jamii na dunia kwa ujumla hapo baadaye. Tunagusa nyanja zote muhimu kama ifuatavyo:
Shule ya Sekondari St Monica Wasa ni mahali sahihi kwa ajili ya elimu bora itakayompa mwanao mwanga wa maisha.
Shule imejikita kutoa malezi stahiki yatakayomfanya mtoto/mwanafunzi akubalike katika jamii yote.
Shule inamwandaa mwanafunzi kujitegemea kwa kupata stadi mbalimbali za maisha ikiwemo ufugaji na kilimo.
Wasiliana nasi sasa...!